Wakaazi Wa Soilo Kaunti Ya Nakuru Waliandamana Kuzuilia Mfanyabiashara Mmoja Kujaribu Kujenga Kwa Ardhi Ya Umma Eneo Hilo.
Wakaazi Hao Wanashikilia Kuwa Bwenyenye Huyo Amejaribu Kunyakua Ardhi Hiyo Mara Kadhaa Na Sasa Wameitaka Wizara Ya Ardhi Kaunti Ya Nakuru Kuingilia Kati. Wakaazi Hao Wameshikilia Kuwa Hawatamruhusu Kujenga Kwa Ardhi Hiyo Hadi Pale Ataonyesha Stakabadhi Muhimu Ya Kudhibitisha Madai Yake.