Waziri Wa Elimu Profesa George Magoha Amesema Serikali Itahakikisha Kuwa Kuna Miundombinu Na Vifaa Vya Kutosha Vya Ujenzi Wa Madarasa Kabla Ya Uchaguzi Mkuu Kuwadia.
Akizungumza Katika Ukaguzi Wa Ujenzi Wa Madarasa Ya Mtaala Wa Cbc Katika Shule Ya Upili Ya Wasichana Ya Nyawara Katika Kaunti Ndogo Ya Gem. Magoha Amesema Kuwa Ni Jukumu Lake Kuhakikisha Awamu Ya Pili Ya Programu Ya Maendeleo Ya Ujenzi Utaanza Mwezi Aprili Mwaka Huu, Ili Kuhakikisha Kunakuwa Na Vyumba Vya Madarasa Vya Kutosha Kwa Ajili Ya Wanafunzi Hao Kupita Katika Shule Za Sekondari Za Awali.