Naibu Rais William Ruto Ameandaa Mkutano Na Wajumbe Kutoka Samburu Na Kajiado Nyumbani Kwake Mtaa Wa Karen, Alikowaomba Kuungana Naye Katika Azma Yake Ya Kuwania Urais Wa Nchi Mwaka Ujao. Ruto Amewasuta Wapinzani Wake Kwa Kutowapa Wakenya Suluhu La Kiuchumi Huku Akifafanua Umuhimu Wa Mfumo Wa Kiuchumi Wa 'Bottom Up' Kwa Wakenya. Kwenye Kikao Hicho Pia Naibu Rais Ameapa Kusimama Na Maeneo Ya Ibada Iwapo Atashika Usukani Wa Taifa.