HOTUBA YA RAIS DKT. JOHN MAGUFULI KWENYE IBADA YA KUMSIMIKA ASKOFU MKUU WA JIMBO LA ARUSHA.8/4/2018

video bora 2018-04-09

Views 2

Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Askofu Mkuu Mstaafu Lebulu kwa utumishi wake na ushirikiano ulioutoa kwa Serikali katika kipindi chote cha miaka 20 aliyokuwa Askofu Mkuu na amempongeza Askofu Mkuu Isaac Amani kwa kusimikwa kuliongoza Jimbo Kuu Katoliki la Arusha.
Mhe. Rais Magufuli amemuahidi Askofu Mkuu Isaac Amani, Maaskofu wote na viongozi wote wa madhehebu ya dini hapa nchini kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kushirikiana na viongozi hao katika masuala mbalimbali.
Kwa kunukuu vifungu mbalimbali vya Biblia, Mhe. Rais Magufuli amesisitiza umuhimu wa Watanzania wote wakiwemo viongozi wa dini, Serikali na wanasiasa kudumisha amani, na kwamba Serikali anayoiongoza itakuwa tayari wakati wote kutoa ushirikiano katika kuhakikisha amani inakuwepo.

Share This Video


Download

  
Report form