Rais William Ruto Amejibu Semi Za Kinara Wa Azimio Raila Odinga Ambaye Alidokeza Kuwa Atawahusisha Wakenya Katika Jitihada Zake Za Kuwatetea Makamishna Wanne Wa IEBC. Rais Ruto Amekumbatia Hatua Ya Odinga Ila Hakubaliani Na Jinsi Upinzani Unavyoikosoa Serikali,Kwani Maandamano Si Suluhu Tosha Ya Kuishinikiza Serikali Kuwajibikia Utendakazi Wake.Ruto Hata Hivyo Amemtaka Odinga Kudumisha Amani Katika Maandalizi Ya Vikao Na Ambavyo Amepanga Kuanza Jumatano Wiki Hii. Wabunge Kutoka Mrengo Wa Kenya Kwanza Pia Nao Wameushutumu Mrengo Wa Azimio Kufuatia Hatua Yao Wa Kuwatetea Makamishna Hao Wanne Wa IEBC.