Kulizuka Kizazaa Katika Barabara Ya Migori Kuelekea Kisii Baada Ya Wahudumu Wa Magari Ya Umma Kufunga Barabara Wakilalamikia Ongezeko La Bei Ya Mafuta. Wananchi Hao Wanasema Itakuwa Vigumu Kumudu Hali Ya Maisha Kwani Walikuwa Wakipitia Wakati Mgumu Hata Kabla Ya Ongezeko Hilo. Wanawataka Rais Kenyatta Na Kinara Wa Odm Raila Odinga Kuingilia Kati Ili Kupunguza Madhila Yao.