Rais Kenyatta Aalikwa Tanzania

EbruTVKENYA 2021-12-09

Views 1

Rais Uhuru Kenyatta Yuko Jijini Dar Es Salaam Tanzania, Kujiunga Na Raia Wa Nchi Hiyo Katika Kuadhimisha Miaka 60 Ya Uhuru Wa Taifa Hilo.
Rais Kenyatta, Ambaye Ndiye Mgeni Wa Heshima Katika Sherehe Hiyo, Ni Miongoni Mwa Viongozi Wa Nchi Na Serikali Walioalikwa Na Rais Samia Suluhu Hassan, Maadhimisho Hayo Katika Uwanja Wa Uhuru Jijini Dar Es Salaam, Tanzania. Rais Kenyatta Yuko Jijini Dar Es Salaam,Kama Sehemu Ya Ziara Rasmi Ya Siku Mbili Nchini Tanzania. Akizungumza Na Wanahabari Siku Ya Alhamisi, Balozi Wa Kenya Nchini Tanzania Daniel Kazungu, Alisema Rais Kenyatta Atahudhuria Sherehe Hiyo Kufuatia Mwaliko Kutoka Kwa Rais Suluhu Hassan Mwezi Mei Mwaka 2021, Alipozuru Kenya.

Share This Video


Download

  
Report form