Baadhi Ya Wakaazi Wa Eneo La Mountain View Eneo La Kangemi Wanaendelea Kukadiria Hasara Kubwa Baada Ya Moto Kuteketeza Nyumba Zao. Mamia Ya Wakaazi Wamesalia Bila Makao Huku Wakichukua Fursa Ya Siku Ya Leo Kukusanya Mabati Na Bidhaa Zilizosalia Wakitafakari Jinsi Watakavyoanza Maisha Upya. Wengi Tuliozungumza Nao Wanaitaka Serikali Kuingilia Kati Mara Moja Na Kuwapa Msaada Wa Malazi, Chakula Na Dawa Na Hususan Kuwasaidia Watoto Wao Kwani Sare Na Vitabu Vyao Vimeteketea Katika Moto Huo.