Wizara Ya Afya Sasa Imewaruhusu Watu Walio Na Umri Zaidi Ya Miaka Hamsini Na Minane Kuanza Kuchanjwa.Hatua Hiyo Imechukuliwa Baada Ya Data Ya Maambukizi Kuonyesha Kuwa Wanachangia Asilimia Sitini Ya Wanaofariki Dunia Kutokana Na Makali Ya Covid-19. Katika Taarifa, Mwenyekiti Wa Kamati Ya Utoaji Wa Chanjo Ya Covid-19, Daktari Willis Akwale, Amesema Agizo Hilo Linalandana Na Mapendekezo Ya Shirika La Afya Duniani.