Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC leo imepata ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Stand United katika mchezo wake wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa leo kwenye Dimba la Taifa Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Mrisho Ngasa dakika ya 2, Ibrahim Ajib dakika ya 32, Andrew Vincent dakika ya 35 na Deus Kaseke dakika ya 57, huku mabao yote ya Stand United yakifungwa na Alex Kitenge dakika za 15, 59 na 90+2.
Haya ndiyo mabao yote saba kwenye mchezo huo.