Makachero kumhoji Gavana wa Migori Okoth Obado wakati wowote

Hottest Videos en 2018-09-08

Views 4

Maafisa wa upelelezi wa jinai sasa wanatarajiwa kumhoji gavana wa Migori Okoth Obado, ili kubaini iwapo alihusika na mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo Sharon Otieno, huku ikibainika kwamba mwendazake aliwasiliana na gavana huyo mara sita siku aliyotekwa nyara.
K24 saa moja aidha imebaini kwamba siku aliyotekwa nyara, Sharon alituma ujumbe mfupi kwa gavana Obado na kuuliza ni kwa nini haki zake zilikuwa zikihujumiwa, huku K24 ikibaini pia kwamba huenda genge haramu la gaza lenye makao yake eneo la Kayole jijini Nairobi, lilitumiwa kutekeleza mauaji.

Share This Video


Download

  
Report form