Mahakama ya upeo imezima matumaini ya kuifanyia marekebisho katiba ya nchi kupitia mwafaka wa kisiasa maarufu kama 'Handshake'. Majaji sita kati ya saba hao, walitoa uamuzi kwamba Rais hawezi kuongoza shughuli ya kubadili katiba kutumia sheria ambayo ilitengewa mwananchi wa kawaida.