Ni Afueni Kubwa Kwa Wakaazi Wa Maatha- Gesi Eneo Bunge La Fafi Kaunti Ya Garissa Baada Ya Serikali Kukamilisha Ujenzi Wa Kisima Cha Maji Eneo Hilo. Eneo Hilo Linakumbwa Na Ukame Na Wakaazi Hulazimika Kutembea Muda Mrefu Kutafuta Maji Ya Kunywa Na Matumizi Ya Nyumbani. Kisima Hicho Kinachotoa Maji Lita Elfu 30 Kwa Saa Moja Sasa Kitawahudumia Wakaazi Hao Pamoja Na Mifugo Wao.