Ndege Za Kwanza Kutoka Nairobi Zatua Mombasa Na Kisumu

EbruTVKENYA 2020-07-16

Views 6

Kenya Imerejelea Safari Za Ndege Ndani Ya Nchi Huku Ndege Ya Kwanza Ya Kq Ikianza Safari Kutoka Nairobi Kwenda Mombasa Asubuhi Ya Leo. Ndege Hiyo Ya Kwanza Iliondoka Uwanja Wa Jkia Saa Nne Na Robo Asubuhi Baada Ya Waziri Wa Uchukuzi James Macharia Kuongoza Hafla Ya Kuanzisha Safari Hiyo. Ndege Nyingine Ndogo Ya Kq Ilitoka Nairobi Kwenda Kisumu. Akizungumza Katika Wakati Wa Uzinduzi Wa Safari Hizo, Macharia Alisema Kenya Sasa Inatarajia Kuanza Safari Za Kimataifa. Rais Uhuru Kenyatta Alitangaza Kwamba Safari Za Ndege Ndani Ya Nchi Zitaanza Julai Tarehe Kumi Na Tano Ilhali Zile Za Kimataifa Zitaanza Agosti Mosi. Safari Hizo Zitaendeshwa Kwa Kufuata Masharti Yote Na Mwongozo Wa Wizara Ya Afyana Mamalaka Ya Kusimamia Safari Za Angani.

Share This Video


Download

  
Report form