Kamati maalum iliyoteuliwa na seneti kuendesha mchakato wa kumbandua gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru imekanusha madai ya kushawishika wala kuhongwa kama njia moja ya kumtetea gavana huyo. Kamati hiyo iliyofanya kikao cha kwanza baada ya kuteuliwa,aidha kimemchagua seneta wa kaunti ya Kakamega Cleophas Malala kama mwenyekiti akisaidiwa na seneta Mteule Abshiro Halake.