MAGUFULI AMVUA NGUO MBUNGE WA CHADEMA MBELE YA WANANCHI WAKE

Best Video en 2018-09-07

Views 15

Mbunge wa Serengeti kupitia CHADEMA, Marwa Chacha Rioba, amebabaika na kushindwa kujibu swali la Rais Dk. John Pombe Magufuli juu ya matumizi ya fedha za Mfuko wa Jimbo, Tsh milioni 58 kwa mwaka, baada ya kudai kuwa, alizitumia kujenga kwenye Shule, ikiwemo kusomba mchanga kwa kutumia lori lake.
Hata hivyo, Rioba alizomewa na wananchi waliohudhuria na kujikuta akishindwa kuendelea na kuhamaki kuwa: "Na mimi naweza kuwa Mwana-CCM."

Hiyo imekuja baada ya Rais Magufuli kumuita Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti aje ajibu tuhuma za kula milioni 20. Hata hivyo, DED alifafanua kwa ubora na kukana kutumia fedha nje ya utaratibu. Hali hiyo ilipelekea Rais kumuita Mbunge ili aje afafanue namna alivyotumia fedha milioni 58 za Jimbo. Dah!! Rioba alishindwa kabisa kulijibu swali hilo hadi kuonyesha jinsi alivyotumia lori lake kusomba mchanga. Rais Magufuli alimuonea huruma na kumkatisha asiendelee baada ya Mbunge kuanza kuzomewa.
Hata hivyo, baadaye Rais alitania na kudai kuwa, Mbunge wao amesema ukweli kwa kuwa sura yake ni CHADEMA na mioyoni ni CCM.

Share This Video


Download

  
Report form